Proverbs 31

Misemo Ya Mfalme Lemueli

1 aMisemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

2 b“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu,
ee mwana wa nadhiri zangu,
Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu.

3 dUsitumie nguvu zako kwa wanawake,
uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.

4 e“Ee Lemueli, haifai wafalme,
haifai wafalme kunywa mvinyo,
haifai watawala kutamani sana kileo,
5 fwasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru
na kuwanyima haki zao wote walioonewa.
6 gWape kileo wale wanaoangamia,
mvinyo wale walio na uchungu,
7 hWanywe na kusahau umaskini wao
na wasikumbuke taabu yao tena.

8 i“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,
kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.
9 jSema na uamue kwa haki,
tetea haki za maskini na wahitaji.”

Maneno Ya Mwisho: Mke Mwenye Sifa Nzuri

10 kMke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata?
Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.

Mithali 31:10-31 imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

11 mMume wake anamwamini kikamilifu
wala hakosi kitu chochote cha thamani.
12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya,
siku zote za maisha yake.
13 nHuchagua sufu na kitani
naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara
akileta chakula chake kutoka mbali.
15 oYeye huamka kungali bado giza
huwapa jamaa yake chakula
na mafungu kwa watumishi wake wa kike.
16Huangalia shamba na kulinunua,
kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.
17Hufanya kazi zake kwa nguvu,
mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.
18Huona kwamba biashara yake ina faida,
wala taa yake haizimiki usiku.
19Huweka mikono yake kwenye pia,
navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.
20 pHuwanyooshea maskini mikono yake
na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.
21 qTheluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake,
kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.
22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake,
yeye huvaa kitani safi na urujuani.
23 rMume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji,
aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.
24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza,
naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25 sAmevikwa nguvu na heshima,
anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.
26Huzungumza kwa hekima
na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.
27 tHuangalia mambo ya nyumbani mwake
wala hali chakula cha uvivu.
28 uWatoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa,
mumewe pia humsifu, akisema:
29“Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri,
lakini wewe umewapita wote.”
30 vKujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi,
bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.
31Mpe thawabu anayostahili,
nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.
Copyright information for SwhNEN